Simba yateswa na rekodi yake

Tuesday June 22 2021
simba pic
By Olipa Assa

SIMBA kwa sasa inahesabu siku chache tu kabkla ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa nne mfululizo, lakini ikiendelea kuteswa na rekodi waliyoiweka msimu wa 2018-2019.

Katika msimu huo, Simba ilimaliza ligi ikiwa na pointi nyingi zilizobaki kuwa rekodi hadi sasa kwenye ligi hiyo, kwani ilikusanya alama 93 na mbao 77 katika mechi 38 na kuvunja rekodio iliyokuwa ikishikiliwa na Yanga msimu wa 2015-2016 ilipomaliza msimu na pointi 73 na mabao 70. msimu uliopita, Simba ilishindwa kuifikia rekodi hiyo kwani ilibeba ubingwa na pointi 88 kwa idadi ya mechi kama hizo pamoja na mabao 78 ikiweka rekodi mpaka sasa katika msimu mmoja.

Ukiangalia msimu wa sasa, Simba ina nafasi kubwa ya kubeba ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo, lakini haitakuwa na jeuri ya kuifikia rekodi hiyo ya misimu miwili iliyopita na kama itachemsha kwenye mechi ilizosaliwa nazo kwa sasa msimu huu inaweza isiifike ya msimu uliopita.

Ndio, Simba kwa sasa ina alama 70 baada ya mechi 28, ikisaliwa na michezo sita mkononi ambayo kama itashinda yote itakusanya alama 18 na kuifanya imalize msimu huu na pointi kama za msimu uliopita, lakini ikichemsha mechi yoyote hata kwa sare tu itakwama kuzifikia pointi hizo. Simba pia ina mabao 65 hadi sasa.

Hata hivyo utamu ni kwamba kama Simba itamaliza msimu kwa pointi hizo 88 itakuwa imefanya kazi kubwa kwa vile msimu huu idadi ya mechi zimepungua kutoka 38 hadi 34, ila ubingwa kwao ni lazima hasa kama itashinda kesho dhidi ya Mbeya City kisha kuinyoosha Yanga Julai 3.

Ushindi wa mechi hizo utaifanya Simba iofikisha pointi 76 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyoye, kwani Yanga yenye uwezo wa kfikisha alama kama hizo, kama itapasuka Julai 3, maana yake ikishinda mechi mbili itakazobakiwa nazo itafikisha alama 73 tu (kama jana iliifunga Mwadui pia).

Advertisement

Yanga imebakiza mechi nne sawa na pointi 12 ambazo ukizijumlisha na 64 zinapatikana alama 76. wakati wapinzani wao kama watachanga karata zao vyema itamaliza ligi kuu ikiwa na pointi 88.

Namna ligi inavyoelekea kumalizana na hesabu zilivyo zimemfanya aliyekuwa kocha msaidizi wa Gwambina, Athuman Bilali ‘Bilo’, kusisitiza haoni wa kuizuia Simba isiwe bingwa, japo haitafikia rekodi yao ya misimu miwili ilipofunga pia mabao 77 kwani msimu uliopita ilimaliza na mbao 78.

“Utamu wa ligi ni kumficha bingwa hadi mechi ya mwisho kwani endapo kama timu zingekuwa zimecheza mechi sawa, hapo kila mchezaji angekuwa anacheza kwa jasho, lakini kwa sasa Simba ikifikisha pointi 76 itakuwa ina uhakika wa ndoo, pia ikiwa na idadi kubwa ya mabao,” alisema Bilo.

Advertisement