Simba yashusha presha Yanga mbio za ubingwa

SARE ya bao 1-1 kati ya wenyeji Azam FC na Simba imeshusha presha kwa vinara wa ligi kuu bara Yanga baada ya wapinzani wao kudondosha pointi mbili.

Sare ya leo kwenye mchezo huo inaitanya Simba ifikishe pointi 50 ikiwa nyuma pointi 10 kwa mtani wake Yanga huku Azam FC wakifikisha pointi 33 na kuendelea kubaki nafasi ya tano.

Mchezo ulianza kwa timu hizo kusomana dakika tano za mwanzo wenyeji Azam FC walionekana kuwa bora zaidi ya Simba kwa kucheza mchezo wa pasi fupifupi huku Simba wao wakitumia mipira mirefu.

Ubora wa Azam FC kwenye mchezo huo ulithibitishwa dakika ya 36 baada ya Kola kuitanguliza timu yao kupata bao la kuongoza akiunganisha mpira wa aliwatanguliza Azam Lusajo Mwaikenda.

Kola baada ya kupachia mpira nyavuni hakuridi tena uwanjani na nafasi yake ilichukuliwa na Shaban Chirunda.

Simba baadabya kufungwa bao hilo walionyesha kuhitaji bao la kusawazisha kwa kuliandama zaidi lango la wapinzani walitumiq dakika nane tu kusawazisha.

Dakika ya 44 Shomari Kapombe alipiga faulo ambayo iliunganishwa moja kwa moja kwa kichwa na Bocco ambaye amekuwa bora kwenye mechi alizopata nafasi ya kuanza.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika timu hizo zilitoka zikiwa zimefungana bao 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu kila mmoja akitafuta bao la kuongoza ubora wa mabeki wa timu zote mbili ulifanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Dakika ya 61 Prince Dube nusura aiandikie bao la kuongoza timu yake ubora wa mlinda mlango Aishi Manura uliifanya timu hiyo iambulie pointi moja ugenini.

Timu zote mbili zilifanya mabadiliko lakini hayakuwa na madhara kwa pande zote dakika ya 64 alitoka Mudathil Yahya nafasi yake ilichukuliwa na Never Tigere, dakika ya 68 Simba walimtoa Kibo na Bwalya waliingia Peter Banda na Yusuf Mhilu

Dakika 62 Bwalya alionyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea mchezo usio wa kiungwana Bajana, dakika ya 64 alitoka Mudathil Yahya nafasi yake ilichukuliwa na Never Tigere, Simba dakika ya 68 Simba walimtoa Kibo na Bwalya waliingia Peter Banda na Yusuf Mhilu

Dakika ya 76 Banda akiwa na kipa alishindwa kuifungia timu yake bao la kuongoza baada ya kupiga shiti ambalo lilikuwa mboga kwa kipa Salula.

Wakati huo huo dakika ya 81 Bruce Kangwa kaingia Pasco Mshindo katoka Dube kaingia Ayub Lyanga pia alitoka Bajana kaingia Paul Katema wakati kwa upande wa Simba alitoka Bocco nafasi yake ilichukuliwa na Meddie Kagere.

Hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika timu hizo ziligawana pointi moja moja baad ya sare ya bao 1-1 lilifungwa kipindi cha kwanza.