Simba yakomaa na Msauzi

SIMBA iko kwenye mazungumzo na makocha wawili raia wa Afrika Kusini, Eric Tinkle ambaye ni kocha wa zamani wa Maritzburg United na Clinton Larsen wa Polokwane City.
Lakini Mwanaspoti linajua kwamba Larsen ndiye mwenye nafasi kubwa ya kulamba dili hilo.
Habari za uhakika kutoka Sauzi zinasema kwamba Simba imezungumza na mawakala wa makocha hao na dili zote zinakwenda sawa na muda wowote kabla ya Jumatatu lolote linaweza kutangazwa.
Ingawa Tinkle kocha wa zamani wa Maritzburg United na Orlando Pirates ameshtuka baada ya kusikia habari zikimhusisha na Simba, Mwanaspoti linajua dili nzima anaifanya wakala.
Larsen yeye alisema; "Wakala wangu ndiye anayesimamia shughuli kama hizo, ndiye anayeweza kukupa majibu ya kuhusishwa kujiunga na Simba ambao kwasasa hawana kocha mkuu," alisema Larsen.

“Nitasubiri maoni kutoka kwake. Siwezi kukupa maelezo zaidi,"alisema Larsen kwa kifupi huku akiongeza kuwa kama atapata dili kwenye nchi ambayo corona haiko juu atakwenda,"