Simba yaitega Sportpesa kimtindo, Barbara atoa siri

Sunday November 21 2021
Sportpesa PIC

Ofisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez.

By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Klabu ya Simba ni kama imeitega Sportpesa kwenye mkataba mpya wa udhamini baada ya huu wa sasa kuelekea ukingoni mwaka huu.

Kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo leo Jumapili, Ofisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez amefichua mkataba wao na Sportpesa unaelekea kuisha mwishoni mwa mwaka 2021.

"Mwaka huu mkataba wetu na Sportpesa unakwisha, hivyo katika mkataba mpya tutawapa kipaumbelelakini kama tutashindwana kwa thamani ya Simba, tutatafuta mdhamini mwingine," amesema Barbara.

Sportpesa imekuwa mdhamini mkuu wa klabu ya Simba kwa misimu kadhaa, na kwa mujibu wa Barbara mwaka huu mkataba huo unafikia tamati na watakaa kufanya mazungumzo kwa ajili ya mkataba mpya.

Advertisement