Simba wanaishi sana

Muktasari:

UMEONA hii hoteli hapa. Ni ya kishua sana. Ndipo Mnyama alipofikia. Simba wamejaribu kuifunga Kaizer Chiefs nje ya uwanja baada ya kuiweka timu yao katika mazingira mazuri kuelekea katika pambano lao la leo dhidi ya wababe hao wa Afrika Kusini baada ya kuiweka timu yao katika hoteli ya kifahari eneo la matajiri la Sandton.

Msafara wa wababe hao wa Msimbazi umefikia katika hoteli ya Sky iliyopo eneo la kifahari zaidi katika jiji la Johannesburg Sandton ambalo klabu nyingi kubwa duniani pamoja na timu ya taifa hufikia.

Gharama za chumba kimoja katika hoteli ambayo Simba imefikia uanzia dola 200 lakini kutokana na ukosefu wa watalii nchini Afrika Kusini kutokana na Corona hoteli hizo zimeshuka bei na kwa sasa zinaweza kuanzia dola 100 sawa na Sh230,000.

“Hadhi ya Simba ni kubwa na kwa standadi ambazo tumejiwekea kwa sasa lazima tufikie katika hoteli kama hizi. Hoteli ambayo tulifikia Misri tulipokwenda kucheza na Al Ahly ilikuwa nzuri pia kama hii,” alisema Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu. Bahati nyingine nzuri kwa Simba wamefanikiwa kupata uwanja wa mazoezi katika eneo hilo la Sandton ambapo walikuwa wakitumia uwanja wa Discovery Soccer Park.