Simba SC balaa!!

Thursday March 11 2021
SIMBA NOTI PIC
By Thobias Sebastian

KOCHA wa Simba, Didier Gomes amekiri kwamba mastaa wawili waliwaosajili kwenye dirisha dogo, Mnigeria Junior Lokosa na beki wa kati Mzimbabwe Peter Muduhwa ni wazuri lakini wana mtihani mzito.

Mpaka sasa hakuna hata mmoja kati yao aliyecheza mechi yoyote katika kikosi hicho cha Msimbazi licha ya kutua kwa mbwembwe lakini moja ya masharti waliyopewa ni kukomaa zaidi haswa mazoezini ili wapewe nafasi kimataifa ambako ndiko kibarua chao kinaposoma.

lusako

Kiufundi mazoezini pamoja na tathmini za wakuu wa ufundi wa Simba, Lokosa bado hayupo fiti kimwili na Muduhwa anashindwa kucheza kutokana na Pascal Wawa pamoja na Joash Onyango kuelewana tayari.

Kocha wa Simba, Didier Gomes alisema: “Lokosa alishindwa kucheza mechi zenye ushindani kwa muda mrefu kutokana na kule alikokuwa ligi haikuwepo kwa sababu ya corona, kwahiyo mpaka muda anafika hapa hakuwa na utimamu wa mwili.

“Nahitaji muda zaidi wa kumtengeneza Lokosa na kurudisha utimamu wake wa mwili na baada ya hapo ndio nimpatie nafasi ya kucheza, ndio maana mpaka sasa hajaonekana katika mechi za mashindano,” alisema.

Advertisement

“Muduhwa amekuwa akifanya vizuri hata mazoezini lakini inakuwa ngumu kupangua wachezaji ambao wanacheza vizuri na kuelewana katika ligi lakini kama itatokea changamoto au mahitaji zaidi nafasi ya kucheza inawezekana.

“Baada ya msimu kumalizika tutafanya tathmini ya kikosi kizima na kuangalia mahitaji ya timu yetu baada ya hapo ndio nitatoa mtazamo wangu wachezaji ambao tunatakiwa kubaki nao na maeneo ya kuongeza nguvu,” alisema Gomes.

Kwa mujibu wa Gomes ubora ambao wanaonyesha mastraika watatu wa Simba, Chriss Mugalu, John Bocco na Meddie Kagere, Lokosa anahitajika kufanya kazi kubwa na kuonyesha kiwango zaidi kupata nafasi ya kucheza mbele ya mastaa hao.

Advertisement