Simba hakuna kulala Nigeria

Simba yaanza na hili huko Nigeria ni balaaa

Muktasari:

  • Simba iliyojichimbia kwenye hoteli ya nyota nne ya Blue Springs na fasta jioni bila kulaza damu kocha Sven Vandenbroeck, aliwaingiza vijana wake gym iliyopo ndani ya hoteli hiyo.

BAADA ya safari ndefu kutoka jijini Arusha kupitia Ethiopia, kikosi cha Simba kimefika salama mjini Abuja Nigeria na kimeanza kujifua kwa ajili ya mchezo wao wa raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United itakayopigwa Uwanja wa New Jos, mjini Jos.
Simba iliyojichimbia kwenye hoteli ya nyota nne ya Blue Springs na fasta jioni bila kulaza damu kocha Sven Vandenbroeck, aliwaingiza vijana wake gym iliyopo ndani ya hoteli hiyo.
Mapema leo Alhamisi asubuhi kikosi hicho kilipumzika na jioni kimepanga kwenda katika moja ya kiwanja ambacho kipo karibu na hoteli hiyo kufanya mazoezi ya mapesi na mbinu kama sehemu ya kujiandaa na wapinzani wao.
Kikosi hiko cha Simba kesho Ijumaa kitafanya tena mazoezi kwa awamu moja katika uwanja huo aliokuwa karibu na hoteli ya Blue Springs ambao wameukodisha kwa ajili ya kuutumia wao kwa siku mbili tofauti.

Fedha za caf zaipeleka TFF takukuru


Baada ya hapo kikosi cha Simba kitalazimika kuwa njiani kwa umbali wa kilomeya 270, kuwafuata wenyeji wao Plateau FC ambao wapo katika mji wa Jos.
Simba itacheza na Plateau Jumapili Novemba 29, kwenye uwanja wa New Jos uliopo mji wa Jos kuanzia saa 10:00 jioni muda wa Nigeria wakati huku kwetu itakuwa saa 12:00 jioni.
Mratibu wa Simba, Abbas Seleman amesema kikosi hiko kimefika salama na wanaendelea na utaratibu ambao walijipangia kuufanya nchini humo mpaka hapo watakaporejea nchini kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
"Tunamshukuru Mungu kwetu mambo yanakwenda vizuri tupo katika maandalizi ya kuhakikisha tunapambana na kupata kile ambacho tunakihitaji huku ili katika mechi ya marudiano nyumbani tusiwe na kazi kubwa," amesema Seleman.

_________________________________________________________________

Na THOBIAS SEBASTIAN