Samatta akumbuka Mazembe

Tuesday July 20 2021
samatta pic
By Thomas Ng'itu

MSHAMBULIAJI Mbwana Samatta anayeichezea klabu ya Fernabace ameikumbuka jezi yake namba 15 aliyokuwa anaitumia katika kikosi cha TP Mazembe 2011-2016.

Samatta amejikuta akivaa jezi hiyo baada ya kusajiliwa kiungo Mesut Ozil ambaye anapendelea kuvaa jezi namba 10 ambayo alikuwa anaitumia wakati akiwa Arsenal.

Wakati huu wa maandalizi ya msimu mpya, Samatta ameonekana akiwa na jezi hiyo mpya huku Ozil akivaa jezi ambayo ya mshambuliaji huyo wa Tanzania.

Mashabiki wengi wa soka wanasubili kuona makubwa ambayo Samatta atayaonyesha akiwa na jezi hiyo kwani akiwa na Mazembe aliweza kuwa mfungaji bora na mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Advertisement