Rais Samia, Dk Mwinyi kwenye uzinduzi jezi mpya Simba

Klabu ya Simba imezindua jezi zake za msimu wa 2023/24 kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro zikiwa na majina ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Moja ya viongozi majina yao yaliyopo kwenye jezi ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Ra wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, Makamu wa Rais, Philip Mipango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Tulia Ackson.
Jezi yenye rangi nyekundu ikiwa ndio pekee yake iliyopelekwa Kilimanjaro ikiwa na jina la mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji.