Rais CAF akutwa na corona

RAIS wa Shirikisho la soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad amekutwa na virusi vya ugonjwa wa corona baada ya kufanyiwa vipimo Jumatano Oktoba 28, 2020.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Ofisa Habari wa CAF, Alexandre Siewe ilieleza rais huyo kukutwa na covid 19 na kutakiwa kujiweka karantini.

Ahmad aliwasili Cairo, Misri  Jumatano na ndipo alijihisi kuwa na dalili za mafua na kupelekwa katika kitengo maalumu kinachoshughulika na masuala ya covid 19.

“Leo Ijumaa majibu ya vipimo vyake yametoka akigundulika kuwa na virusi hivyo, lakini tayari ameshajiweka karantini yeye mwenyewe kwa siku 14 mbele kwenye hoteli aliyofikia,” ilieleza taarifa hiyo.

“Kwa wale wote ambao walikuwa na ukaribu na Ahmad katika siku saba za nyuma  hasa waliokuwa nae katika safari ya Morocco wanatakiwa wao wenyewe kuchukua tahadhari,”


Covid 19 umeendelea kusumbua baadhi ya nchi, ndani na nje ya Afrika kwa virusi hivyo kuendelea kusambaa kwa hali ya juu.