Pira la Saido litawalaza njaa

Monday October 19 2020
saido pic

MABOSI wa Yanga wamedhamiria kuona msimu huu wanabeba ubingwa baada ya kuukosa kwa misimu mitatu mfululizo ndio maana imeshusha majembe ya maana na kabla dirisha dogo la usajili halijafunguliwa, imemvuta Said ‘Saido’ Ntibazonkiza ambaye kwa mfumo wowote jamaa afiti kikosini.

Dirisha dogo linatarajiwa kufunguliwa Desemba 16 na kufungwa Januari 15 mwakani, lakini Yanga iliamua kumsainisha mkataba wa miaka miwili, mshambuliaji huyo kutoka Vital’O ya Burundi kabla ya kuanza kuitumikia timu hiyo dirisha likifunguliwa, huku ikielezwa huenda asipate tabu kupata namba.

Saido kama atakuwa fiti na kuanza katika kikosi cha kwanza mfumo wa kwanza ambao Yanga inaweza kutumia chini ya Kocha Cedric Kaze ni ule wa 4-4-2, ambao atacheza nyuma ya straika atakayeanza kati ya Michael Surpong, Yocouba Songe au Wazir Junior huku mawinga wakiwa Farid Mussa na Tuisila Kisinda na viungio wakiwapangwa Feisal Salum na Mukoko Tonombe.

Kwa uwezo wake wa kufunga mabao akiwa ndani na nje ya boksi, kumiliki mpira, kupiga vyenga vya mauzi wapinzani na kutengeneza nafasi za kufunga anaweza kufiti na kuingia moja moja katika mfumo huu, kwani akiwa timu ya taifa ya Burundi hucheza kama namba kumi na amekuwa akifunga mabao.

Rekodi zinaonyesha hata alipokuwa akitumikia timu ya NEC (2006-10), aliichezea mechi 70 na kufunga mabao 36, nafasi aliyoichezea pia Cracovia (2010-2014), alipotumika katika michezo 85 na kufunga mabao 31. Mfumo mwingine unaombeba Saido ni ule wa 4-3-3, ambapo kocha anaweza kuanza.

Advertisement