Niyonzima awachana wachezaji wenzake

MCHEZAJI wa Kimataifa wa Klabu ya Yanga Haruna Niyonzima amewataka wachezaji wenzake wa Yanga na wachezaji wengine kukubali presha inayokuwepo katika mbio za ubingwa.

Niyonzima raia wa Rwanda aliyepata nafasi za kucheza timu kongwe za Simba na Yanga aliondoka na kurejea wakati mgumu Yanga ikiwa na presha ya kutwaa taji.

Niyonzima amesema kama kuna mchezaji yoyote ndani ya Yanga hataki kukubali presha zilizopo katika timu yao basi aache kucheza kabisa mpira kwa kuwa presha ni sehemu ya mchezo.

"Presha ni sehemu ya mchezo lakini mimi hainisumbui kabisa, sasa nitashangaa kuona mchezaji hakubali presha akiwa hivyo inabidi aache kabisa kucheza mpira," amesema Niyonzima.

Aidha Niyonzima amesema, toka acheze ligi kuu Tanzania Bara ni mara ya kwanza kuona Yanga ikipitia katika wakati mgumu wa kuchukua kombe la Ligi Kuu mara tatu mfululizo kitendo kinachozidisha presha ya mashabiki ndani ya timu.

"Yanga kukosa ubingwa misimu mitatu mfululizo ndio sababu kubwa inayozidisha presha ndani ya timu na mimi hii ni mara ya kwanza kuwaona Yanga wakikosa kombe mara tatu mfululizo,"