Ninja: Kagere hakuwa na ujanja kwetu

Thursday January 14 2021
niinjaa pic
By Mwanahiba Richard

Beki wa Yanga, Abdallah Shaibu amesema kuwa isingekuwa rahisi kwa straika wa Simba, Meddie Kagere kufurukuta mbele yake hasa akiwa anacheza kwenye ardhi yake ya nyumbani.

Ninja alikuwa sambamba kila hatua ambayo Kagere anapiga katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi ililofanyika juzi Jumatano kwenye uwanja wa Amaan kisiwani hap ambapo Yanga walitwaa ubingwa huo.

ninja kagere pic

Yanga walitwaa ubingwa huo kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya dakika 90 kutoka sare tasa hivyo bingwa kupatikana kwa penati.

Ninja ambaye alipiga penati ya pili kati ya tano zilizokuwa zimepigwa kwa kila timu lakini beki huyo na mwenzake Said Juma Makapu wakimbada vilivyo Kagere aliyeonekana kushindwa kupenya mbele yao.

Ninja alisema kuwa Kagere ni mchezaji mzuri hivyo unapaswa kuwa makini kucheza naye na kutompa nafasi ya kupita anapokuwa kwenye eneo la hatari.

Advertisement

"Nashukuru Mungu nimecheza kadri ya uwezo wangu, nimeaminiwa kupewa penati tena nimeicheza na kufunga, hivyo isingekuwa rahisi kwa Kagere kuchomoka wakati nacheza kwenye ardhi yangu,

"Nawapongeza wachezaji wenzangu kutwaa ubingwa huu maana ni moja ya malengo yetu ya msimu huu, sasa tunajipanga kwa ajili ya mashindano mengine ili tuendelee kufanya vizuri," alisema Ninja

Kocha mkuu wa Yanga, Cedric Kaze alimwamini Ninja tangu mechi ya nusu fainali dhidi ya Azam Fc kumpa nafasi ya kupiga penati ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu atue Yanga, nafasi zote mbili amezitumia vizuri.

yanga znj kaze pic

Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi alielezea hilo kuwa, "Watu hawamwamini Ninja kwneye upigaji penati kwasababu hakuwa kupiga lakini kocha amemwamini na amefundishwa ndiyo maana mecheza vizuri penati zote mbili,".

Advertisement