Ndumbaro mgeni rasmi Simba vs Al Ahly

Friday February 19 2021
NDUMBARO PICHAA\

Wakili Damas Ndumbaro

By Ramadhan Elias
By Thomas Ng'itu

WAZIRI wa Mali Asili na Utalii, Dr Damas Ndumbaro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Jumanne ya wiki ijayo katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Simba inashuka dimbani huku ikiwa na mtaji wa pointi tatu mkononi baada ya mchezo wao wa kwanza ugenini kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya As Vita 1-0.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Ijumaa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Haji Manara amesema mgeni rasmi wao ni Ndumbaro.

"Tunaitangaza nchi na Visit Tanzania, tumewaletea na Waziri mwenyewe", amesema Manara

Manara ametamba kwa kusema kuwa, "Simba ndio tunaiwakilisha Afrika Mashariki kwa kuitangaza, tunatangaza nchi pamoja na ukanda wote hakuna timu yoyote iliyopo katika hatua hii."

Simba hivi karibuni ilianza kuitangaza nchi kwenye michuano hiyo baada ya kuingia ubia na wizara hiyo kwa kuvaa jezi zilizoandikwa Visit Tanzania.

Advertisement
Advertisement