Nchimbi arejea kikosi cha kwanza

Tuesday April 20 2021
nchimbi pic
By Thomas Ng'itu

KAIMU kocha mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi amemrejesha katika kikosi cha kwanza mshambuliaji Ditram Nchimbi katika mchezo wao wa leo usiku dhidi ya Gwambina.

Urejeo wa Nchimbi anachukua nafasi Saido Ntibazonkiza ambaye ameanzia benchi katika mchezo huu.

Mwaambusi hajafanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi hiko na kile kilichocheza dhidi ya Biashara UTD na kushinda 1-0 mchezo uliochezwa wiki iliyopita katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha huyo amemuanzisha Faruk Shikhalo, Kibwana Shomari, Adeyum Saleh, Dickson Job, Abdallah Shaibu, Tonombe Mukoko na Tusila Kisinda.

Wengine ni Carlos Carlinho, Yacouba Sogne, Deus Kaseke na Ditram Nchimbi.

Upande wa benchi wapo Ramadhan Kabwili, Paul Godfrey, Bakati Mwamnyeto, Said Makapu, Haruna Niyonzima, Michael Sarpong na Saido Ntibazonkiza.

Advertisement

Biashara United walioanza: Ibrahim Isihaka golikipa, Rajabu Rashidi, Gustapha Saimoni, Baraka Mtui, Novert Lufunga, Yusuph Kagoma, Meshack Mwita, Yusuf Lwenge, Paulo Nonga, Rajabu Athuman, Japhet Mayungu.

Advertisement