Nabi: Tulieni vitu vinakuja

Summary

BAADA ya kupoteza mchezo dhidi ya Vipers SC ya Uganda, Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi amesema mashabiki wa Yanga wasiwe na presha mambo mazuri yanakuja.

BAADA ya kupoteza mchezo dhidi ya Vipers SC ya Uganda, Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi amesema mashabiki wa Yanga wasiwe na presha mambo mazuri yanakuja.

Mchezo huo ambao umepigwa Uwanja wa Mkapa Jijini Dar kuanzia saa 1:00 usiku, kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Vipers kuongoza kwa bao 1-0, kabla ya kipindi chapili kuongeza lingine.

"Hata mimi nilitamani kupata ushindi kweye mechi hii lakini niseme tu mashabiki wasiwe na hofu,"

Nabi ambaye hivi karibuni ameongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuinoa timu hiyo, amesema kuna baadhi ya mapungufu ambayo ameyaona lakini yote hayo yalitokana na uchache wa siku walizokaa wachezaji kambini.

"Baadhi ya wachezaji wanafanya makosa lakini iiitokana na ukweli kwamba hawakufanya mazoezi kwa muda na niliwaongezea siku za kupumzika kwa sababu msimu uliopita ulikuwa mgumu sana,"alisema Nabi na kuongeza

"Zaidi kwangu ilikuwa ni mechi ya kirafiki na lengo lilikuwa ni kuangalia kile nilichofanyia kazi kambini."