Mukoko kuivaa Stars

Wednesday September 15 2021
TUNOMBE MUKOKO
By Thomas Ng'itu

KIUNGO Mukoko Tonombe amejumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa DR Congo kinachojiandaa kucheza na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar 2022.

DR Congo itacheza na Stars, Septemba 3 mchezo utakaopigwa nchini Congo kisha Septemba 7 wakongo watakuwa ugenini dhidi ya Benin.

Mukoko ambaye anacheza katika klabu ya Yanga nchini, anakuwa sehemu ya kikosi hicho chenye wachezaji 24.

Kiungo huyo amekuwa na wakati mzuri akiwa na Yanga kiasi cha kufanya aitwe mara kwa mara katika kikosi cha DR Congo.

Wachezaji wengine wanaounda kikosi cha DR Congo ni makipa, Joel Kiassumbua, Herve Lomboto na Bagio Siadi

Mabeki ni Joel Ikoko, Mukoko Amale, Christian Luyindama, Chris Mavingq, Chancel Mbemba,Marcel Tisserand, Glody Ngonda na Fabrice Nsakala.

Advertisement

Viungo Edson Kayembe, Mukoko Tonombe,Fabrice Ngoma, Gael Kakuta, Samuel Moutousamy na Neeskens Kabano.

Wakati eneo la ushambuliaji likiwa na Chadrack Akolo, Brit Assombalonga, Cedric Bakambu, Yannick Bolasie, Meshack Elia, Jackson Muleka na Dieumerci Mbokani.

Advertisement