Msuva aukubali mziki wa Kisinda

Friday June 11 2021
TUISILA PIC
By Olipa Assa

KUONDOKA Yanga kwa straika wa kimataifa, Simon Msuva anayekipiga Wydad Casablanca ya Morocco hakumzuii kufuatilia kila kitu kinachoendelea kwenye Jangwani, ndio maana amemtaja, Tuisila Kisinda ndiye anayemkosha na anaamini akiendelea kukaza buti atakuwa tishio.

msuva pic

Msuva aliondoka Yanga akiwa mfungaji bora (mabao 14) msimu 2016/17 ambapo alijiunga na El Jadida aliyoitumikia miaka minne kabla ya kutimkia Wydad Casablanca msimu huu.

Msuva alimtaja Kisinda kwamba ana kitu cha kipekee cha kuisaidia timu hiyo.

Kabla ya kamati ya usajili ya Yanga kumsajiliwa Kisinda msimu huu, lilionekana pengo la Msuva kutozibika tangu alipoondoka Jangwani mwaka 2017 na kitu kikubwa kilichokuwa kikikumbukwa kwake ni mbio zilizokuwa zinasaidia mashambulizi pamoja na kufumania nyavu.

Alisema ni mchezaji mwenye mbio ambazo zitasaidia kuwapa presha wapinzani wao.

Advertisement

“Kisinda ni mchezaji mzuri, huwa namfuatilia na kujua anafanya nini, siwezi kusema moja kwa moja kwamba tunafanana, kwani kila mmoja amejaliwa kitu chake na Mungu, kitu kikubwa na chamsingi ni namna anavyofanya kazi kwa ajili ya kuisaidia Yanga,” alisema Msuva.

Advertisement