Mo Dewji: Hakuna mtu mkubwa zaidi ya Simba

Friday July 30 2021
mkubwa pic
By Ramadhan Elias

Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji “Mo Dewji” amesema kuwa hakuna mtu mkubwa zaidi kuliko klabu hiyo na wote waliopo waliikuta na wataiacha akiwemo yeye.

Mo Dewji ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi mfano wa hundi ya Sh 20 bilioni kwa uongozi wa Simba alizoziahidi hapo awali.

“Hii taasisi inaendeshwa kiuweledi na kwa nidhamu kubwa na siku zote hakuna mtu mkubwa zaidi ya Simba.

Hata mimi ni mdogo kuliko Simba, wote tumezaliwa tunaikuta klabu hii na tutaiacha na wengine watashika nyadhifa tofauti ndani yake,” amesema Mo.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Simba kuachana na aliyekuwa msemaji wao, Haji Manara.

Advertisement