Miamvuli yatawala Uwanja wa Karume

ZIKIWA zimesalia saa chache kwanza kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Biashara United na Simba kwenye Uwanja wa Karume, Musoma miamvuli inaonekana kutawala katika majukwaa ya Dimba hilo.

Tayari mashabiki wa timu zote mbili, wameanza kuingia Uwanjani na kukaa katika jukwaa moja lililopo uwanjani hapo huku wengi wao wakionekana kujifunika miamvuli kutokana na jua kua kali.

Jukwaa  hilo moja la uwanjani hapo limegawanywa katika sehemu mbili ambapo nusu wamekaa mashabiki wa Biashara na nusu nyingine wamekaa mashabiki wa Simba ambao tayari wamekwisha jaza eneo lao.

Mchezo huo wa kwanza wa Ligi Kuu kwa timu zote mbili katika msimu wa 2021/2022 unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 10:00 jioni.