Mchezaji bora Kaizer vs Simba kuoga pesa

Muktasari:

WAKATI Mchezaji tegemeo ndani ya kikosi cha Simba Luis Miquissone akisema yuko tayari kwa mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs Uongozi wake umetangaza kutoa sh  2.5 mil kwa nyota atakayeng'ara katika mchezo huo.

Simba ni wageni wa Kaizer mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa unaotarajiwa kurindima katika uwanja wa FNB Nchini Afrika Kusini.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii Luis ameandika "I'm ready to do my job," akimaanisha yuko tayari kufanya kazi yake, kama wanasimba wanavyoifahamu kazi kubwa ambayo uifanya akiwa ndani ya dakika 90.

Kwa upande wa Simba kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari Haji Manara amesema, kwa kutambua umuhimu na thamani ya mchezo mchezaji bora wa upande wa Simba atajinyakulia pesa hizo.

Amesema utaratibu huo unafanyika katika kila mchezo huku akiwataka mashabiki wa Simba kuendelea kuomba dua ili timu yao iweze kupata matokeo katika mchezo huo.