Mastraika Yanga wapewa mbinu za kuiua Simba

Muktasari:

MICHAEL Sarpong, Fiston Abdul Razack, Wazir Junior, Yacouba Sogne, Tuisila Kisinda na Said Ntibazonkiza ni miongoni mwa washambuliaji wa Yanga ambao wamepewa mbinu za kuiangamiza Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kesho Jumamosi Mei 8.

MICHAEL Sarpong, Fiston Abdul Razack, Wazir Junior, Yacouba Sogne, Tuisila Kisinda na Said Ntibazonkiza ni miongoni mwa washambuliaji wa Yanga ambao wamepewa mbinu za kuiangamiza Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kesho Jumamosi Mei 8.

Mbinu hizo zimetolewa na nyota wa zamani wa Yanga na 'Taifa Stars' Sekilojo Chambua ambaye hadi sasa ndiye anaongoza kwa kufunga mabao mengi kwenye dabi akiwa amepachika jumla ya mabao saba na yote akiifunga Simba.

Akipiga stori na Mwanaspoti Chambua amewaibia siri wachezaji wa Yanga kuwa japo Simba kwa sasa wanaonekana kuwa bora zaidi yao lakini wanafungika endapo watafuata ushauri wake alioutoa hapa.

"Mastraika wa Yanga ndio wanajukumu la kuiua Simba, wanatakiwa kuwa makini na watulivu kwenye kila nafasi ya kufunga watakayoipata ili kuitumia vyema na kufunga.

Wakiweza kutangulia kufunga itawapa nguvu Yanga kwani Simba licha ya kuwa na wachezaji wengi bora lakini wataanza kucheza kwa presha kubwa jambo ambalo litawafanya wakose maelewano mazuri," alisema Chambua na kuongeza:

"Wote tumecheza mpira hivyo presha ya kutangulia kufungwa tena kwenye mechi kubwa kama hiyo tunaijua, hivyo basi utulivu wa hali ya juu, kijuiamini na kujitoa kwaajili ya timu kwa washambuliaji na wachezaji wengine wa Yanga ndivyop vitawafanya kuibuka na ushindi katika mechi ya Jumamosi," alisema.

Chambua ni miongoni mwa wachezaji waandamizi wa Yanga kwani alijiunga na wanajangwani hao mwaka 1994 na kuichezea timu hiyo hadi kustaafu kwake mwaka 2002.

Baada ya hapo alikuwa kocha msaidizi wa timu hiyo  chini ya kocha mkuu raia wa Malawi Jack Chamangwana (Marehemu) kuanzia mwaka 2002 hadi 2004.