Mashabiki Yanga wagoma kisa TFF

Mashabiki wa Yanga wakilalamika baada ya muda wa mechi yao dhidi ya Simba kusogezwa mbele. Picha na Michael Matemanga

MASHABIKI wa klabu ya Yanga wameonyesha kuchukizwa baada ya mechi yao dhidi ya Simba kusogezwa mbele.

Awali mchezo huo ulitakiwa uchezwe leo saa 11:00 jioni lakini ilipofika saa 8 mchana ilitoka taarifa katika Shirikisho la mpira wa miguu TFF ikisema mchezo huo umesogezwa mbele mpaka saa 1:00 usiku.

Mashabiki hao waliokuwa wamevaa jezi za Yanga walisogea mpaka katika mlango wa waandishi wa habari na kuanza kitoa kero zao.

Kero zao kubwa walizokuwa wanazitoa walikuwa wanahoji kwanini mchezo huo umesogezwa mbele.

“Mchezo ulikuwa unajulikana ni saa 11 sasa iweje wasogeze mbele, ndugu muandishi kwani kanuni zinasema hivyo? au ni mipango tu,” walisikika mashabiki hao waliojitokeza kwa wingi.