Mashabiki wamkataa Sarpong

Muktasari:

Kama kuna mchezaji ana wakati ngumu katika mchezo wa leo  wa Yanga dhidi ya Namungoa basi ni Michael Sarpong baada ya mashabiki kupiga kelele atolewe.

Kama kuna mchezaji ana wakati ngumu katika mchezo wa leo  wa Yanga dhidi ya Namungoa basi ni Michael Sarpong baada ya mashabiki kupiga kelele atolewe.

Saporng ameonekana kutokuwa na msaada dakika 45 za kipindi cha kwanza kiasi cha mshabiki kutaka atolewe.

Mchezaji huyo raia wa Ghana ameanza sambamba na Yacouba Sogne lakini licha ya kazi nzuri inyofanywa na Tuisila Kisinda na Said Ntibazonkiza 'Saido' ya kuwalisha mipira washambuliaji hao lakini wameshindwa kufunga.

Sarpong ndio amewatia hasira zaidi mashabiki kwani ameongoza kupoteza pasi na kupokonywa Mpira kirahisi Jambo ambalo wanaamini limewakosesha Yanga ushindi kipindi cha kwanza.

Licha ya Yanga kufanya mashambulizi mengi langoni kwa Namungo lakini mipira Mingi inapofika kwa Sarpong Imekuwa ikichukuliwa na timu pinzani hivyo mashabiki kushindwa kuvumilia na kuanzia kupiga Kelele toa huyo.. toa huyoo.

Hata baada ya filimbi ya mwamuzi Hance Mabena kuashiria ni mapumziko, na wakati wachezaji wakirudi vyumbani bado mashabiki walionekana  kumtaka kocha amtoe Sarpong