Mashabiki Namungo nao hawapoi, waipania Yanga

Mashabiki wa Namungo wa tawi la Ruangwa mjini wamesema kuwa Yanga huwa haiwasumbui wanapocheza nayo kwenye uwanja wa Majaliwa hivyo Leo watahakikisha wanamaliza kabisa ndoto zao za ubingwa.

Uwesu Salim ambayo ni shabiki kindakindaki wa timu hiyo amesema kutokana na washambuliaji wakali waliopo katika kikosi Cha Namungo lazima washinde mechi ya Leo.

"Yaani nawahurumia mabeki wa Yanga watalala na viatu Leo maana tuna

 washambuliaji hatari wakiongozwa na Stephen Sey,Reliants Lusajo na Shiza Kichuya.

"Hawatoki na Leo zile ndoto zao za ubingwa ndio tunazimaliza kabisa kwani lazima waziache pointi zote hapa Ruangwa,"amesema Uwesu.

Naye shabiki mwingine Muksin Mteta amesema Yanga huwa haiwasumbuhi wanapokutana kwenye uwanja wa Majaliwa hivyo hata Leo lazima wapigwe.

"Hatunaga presha na Yanga sisi, hata wenyewe wanajua shughuli yetu wakija hapa kwetu hivyo wajipange.

"Leo tunashinda na mpira tunawapigia vile vile,hawana ubavu wa kutufunga ," amesema Mteta.

Naye  Ahmad Issa amesema leo wanawapiga Yanga mabao 3-0 yatakayofungwa na Sey,Lusajo na Kichuya.

"Nawaamini washambuliaji wetu wako vizuri na hiyo mechi lazima tushinde mabao matatu kwa bila na yatafungwa na Sey,Kichuya na Lusajo,"amesema Issa.