Mashabiki bado Sokoine

Mbeya. Pamoja na milango kufunguliwa mapema, lakini mashabiki na wadau wa soka wameonekana kusuasua kuingia uwanjani kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu kati ya Mbeya City na Simba.

Mechi hiyo ya kiporo inatarajia kupigwa saa 10 jioni katika uwanja wa Sokoine jijini hapa.

Milango ilifunguliwa tangu saa 4 asubuhi, lakini hali imeonekana kuwa tofauti kwa mashabiki na wadau kuhamasika kuingia uwanjani.

Mwanaspoti imepenya ndani ya uwanja huo na kuona majukwaa yakiwa 'kavu' bila shabiki yeyote japokuwa uuzaji tiketi unaendelea.

Haijajulikana haraka wanaonunua tiketi wanapotelea wapi huku ikidhaniwa kuwa huenda wanasubiria muda wa kukaribia na mechi kuweza kuzama uwanjani.