Lwandamina ni suala la muda kutua Azam FC

Lwandamina ni suala la muda kutua Azam FC

Muktasari:

KOCHA wa zamani wa Yanga, George Lwandamina huenda akachukuwa nafasi ya Aristica Cioaba aliyefungishiwa virago hivi karibuni Azam FC.


THOMAS NG'ITU

KOCHA wa zamani wa Yanga, George Lwandamina huenda akachukuwa nafasi ya Aristica Cioaba aliyefungishiwa virago hivi karibuni Azam FC.

Habari za ndani kutoka ndani ya Azam FC, zinasema kwamba mabosi wa timu hiyo wamefanya mazungumzo na kocha huyo aliyewahi kuifundisha Zesco ya Zambia ambapo muda wowote anatua nchini kwa ajili ya kusaini mkataba.

Lwandamina hatakuwa mgeni na Ligi Kuu Bara kwani aliifundisha Yanga misimu miwili kuanzia 2016-2018, hivyo anaielewa ligi ilivyo pamoja na changamoto zake.

"Amezungumza na viongozi kila ktu ambapo mazungumzo yao yameenda vizuri, lakini kusaini mkataba mpaka aje nchini," kimeeleza chanzo hicho.

Imedaiwa Lwandamina alikuwa na dili la kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya Prison Leopards lakini ameachana nalo kutokana na ofa ya Azam FC.

Mwanaspoti Online lilizungumza na kocha huyo kutoka kwao Zambia juu ya ujio wake ambapo alijiubu kwa ufupi tu kwamba; "Nakuja Tanzania hivi karibuni,"