Laivu kutoka karantini ya mastaa wa Namungo

Namungo: Wasudan hawachomoki nyumbani

KIUNGO wa Namungo, Lucas Kikoti amezungumza na Mwanaspoti laivu kutoka alikowekwa karantini nchini Angola.

Amesema yeye na wenzake wako poa walikoshikiliwa wakidaiwa kuwa na mambukizi ya Covid19 huku akiwataka wenzake kupambana kesho na kuhakikisha wanaichapa Premiero de Agosto.

Namungo itacheza na Premiero de Agosto Jumapili kwenye uwanja wa Chamazi katika mchezo wa hatua ya mtoano wa Kombe la Shirikisho Afrika kisha timu hizo zitarudiana Februari 25 hapa hapa nchini.

Mchezo wa kwanza baina ya timu hiyo uliokuwa ufanyike Februari 14 nchini Angola ulishindwa kufanyika kutokana na Namungo kukutana na figisu nchini humo huku wachezaji watatu wa timu hiyo akiwemo Kikoti, Fred Tangalu, Khamis Fakhi pamoja na Mtendaji mkuu, Omari Kaya kushikiliwa kwa madai wamepimwa na kukutwa na maamubukizi ya Covid 19.

Kutokana na hali hiyo Shirikisho la Soka Afrika (Caf) lilifuta mchezo huo na baadae kutoa maamuzi kuwa michezo yote miwili baina ya timu hizo ifanyike Tanzania.

Kikoti anaamini kuwa timu yao ni bora na itashangaza huku akiwataka wenzake kucheza kwa bidii ili kupata ushindi katika michezo yote miwili na kuwapa faraja wao na pia kuipa manufaa nchi.“Sisi bado tuko Karantini huku Angola na tunaendelea vizuri hatuna tatizo lolote hivyo hatujua tutarejea lini Tanzania tunachosubiri ni uamuzi wao. Ila wanatuhudumia vizuri tu wakitupa kila tunachohitaji.