KWAKO KASHASHA: Zijue sifa za kikosi kipana katika soka

Saturday October 24 2020
kashasha pic

Mara nyingi timu inaundwa na wachezaji mbalimbali au wachezaji mchanganyiko.

Kiutaratibu timu zinakuwa zinapewa angalau nafasi ya kusajili wachezaji 30 kama ilivyo hapa kwetu na hili linafanyika kwa kuzingatia idadi ya mashindano, majeruhi na sababu nyinginezo na Tanzania kama ilivyo kwa baadhi ya nchi, Tanzania pia nadhani iko kanuni hiyo. Siku za hivi karibuni kumekuwa na dhana a,a tafsiri ya neno ‘kikosi kipana’ ambayo imekuwa ikitumiwa na timu pale inapokuwa imefanya usajili wa kundi kubwa la wachezaji.

Lakini inawezekana watu wakawa wanazungumzia dhana ya kikosi kipana, sasa tujaribu kuona sifa za timu yenye kikosi kipana ni zipi. Sifa ya kwanza ni lazima uwe na wachezaji wanaofanana au kukaribiana au quality ama attributes na hapa tunaangalia qualities tatu za muhimu.

Ya kwanza tunaita TTQ ambayo ni technical and tactical quality na pili ni mental qualities na la tatu ni physical qualities. Sifa ya pili ya timu yenye kikosi kipana uhakika wa kuwa na wachezaji wenye kiwango kikubwa cha uelewa wa mchezo wenyewe. Ni lazima wachezaji wawe na uwezo wa kufanya interpretation ama utafsiri wa mchezo ulivyo na pia mbinu ambazo wanapewa na benchi lao la ufundi.

Kigezo kingine cha timu inayotakiwa kujinasibu kuwa ina kikosi kipana ni uzoefu na exposure inayofanana. Ukiwa na wachezaji wa namna hii inasaidia kuzibiana mapungufu pale mmojawapo anapokuwa amekosea au ana udhaifu fulani katika mchezo. Sifa nyingine ambayo timu yenye kikosi kipana intakiwa kuwa nayo ni lazima iwe na wachezaji angalau wawili wa nafasi moja ambao kiwango chao wanakaribiana. Hiki ndicho kigezo ambacho timu nyingi zimekuwa zikikitumia kujisifia kuhusu mtazamo wa kuwa na kikosi kipana. Pamoja na hizo, timu yenye kikosi kipana pia inatakiwa kuwa na kundi kubwa la versatile players. Hawa ni wachezaji ambao wana uwezo na sifa kubwa ya kucheza zaidi ya nafasi moja uwanjani. Unapokuwa na wachezaji kama hawa, unakuwa na uhakika wa kuzibwa kwa nafasi za wachezaji wengine pindi wanapokosekana ama kwa majeraha au sababu nyingine.

Kwa hiyo tunapozungumzia dhana ya kikosi kipana kwa timu tunapaswa kuvitazama vigezo ama sifa hizo zilizoainishwa hapo juu.

Advertisement

Kaze apewe muda Yanga

Juzi tumeiona Yanga ikicheza mechi yake ya kwanza ikiwa chini ya Kocha Mkuu mpya, Cedrick Kaze kutoka Burundi ambaye yeye timu hiyo imemchukua kuziba pengo la Zlatko Krmpotic aliyetimuliwa hivi karibuni.

Nilichokiona ni mapema mno kuanza kumjadili kocha Kaze kwa kuangalia mchezo ule wa juzi ambao walicheza dhidi ya Polisi Tanzania na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwani anahitaji muda wa kuitengeneza zaidi timu, jambo ambalo haliwezi kutimia ndani ya muda mfupi. Hata hivyo yapo baadhi ya mambo ambayo yameonyesha taswira kuwa Kaze atayafanya ndani ya kikosi cha timu hiyo kwa siku za usoni ambayo kupitia mchezo wa juzi dhidi ya Polisi, wengi watakuwa wameyang’amua.

Miongoni mwa mambo ambayo nimeyaona kwa Kaze ni kwamba anataka kuona timu inacheza mpira wa chini ili wachezaji wote waweze kushiriki kuuchezea mpira. Mkicheza mpira wa chini inakuwa ni rahisi kwa kundi kubwa la wachezaji kuuchezea tofauti na iwapo mnapocheza mpira wa juu ambao ni wachezaji wachache tu watakaonufaika kutokana na kutofautiana kwa maumbile. Hata hivyo ufanisi katika kufanyia kazi staili hiyo ya Kaze ulionekana kutokuwa juu na hilo bila shaka linachangiwa na ugeni wa wachezaji kwa staili hiyo ukizingatia kwamba kwa sasa wanabadilisha kutoka utamaduni waliouzoea kwenda katika utamaduni mpya.

Moja ya changamoto ambazo zilionekana kwa staili hiyo mpya ni wachezaji kupoteza mipira lakini pia unaweza kuona mchezaji kama Yassin Mustafa akishindwa kuover lap kama alivyozoea na hiyo ni kwa sababu hakukuwa na ule upigaji wa mipira mirefu.

Ili kuiona Yanga ikicheza soka safi na la kuvutia, inahitaji muda kwa sasa wapo katika transition ya kutoka kwenye matumizi ya high balls kwenda katika matumizi ya mipira ya chini. Ukicheza mipira ya juu unatakiwa kuwa na aerial skills na sasa wanaenda kuwa na matumizi ya grund skills. Akipewa muda nadhani ataweza kufanya vizuri zaidi siku za usoni.

Ushindani wa Ligi Kiboko

Kwa upande mwingine, Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ingawa ipo katika raundi ya saba (7), imeonyesha kuwa ngumu na yenye ushindani na hii imetokana na kuanza kubadilika kwa malengo ya timu kwa sababu mnapoanza ligi, wote mnakuwa na lengo moja lakini kadri mnavyocheza, malengo yanaanza kubadilika.

Kitendo cha kubadilisha makocha kwa baadhi ya timu kinatoa ishara kwamba viongozi wa klabu wapo serious na wana commitment na wanaonyesha kwamba tayari presha ya kutofanya vizuri imeanza kuwapata hivyo wanaona bora waanze kuchukua hatua ili timu ziwe katika mstari sahihi.

 

Advertisement