Kwa Mkapa changamoto kwa wachezaji Simba v Kagera

Saturday May 01 2021
uwanja pic
By Olipa Assa

UWANJA wa Benjamin Mkapa, kuwa na maji kutokana na mvua zinazonyesha katika jiji la Dar es Salaam ni changamoto kwa wachezaji wa Simba na Kagera Sugar kuonyesha soka la ufundi.

Simba na Kagera Sugar, zinacheza mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam, timu itakayopigwa itakuwa imeaga michuano hiyo.

Wachezaji wanaonekana kupata shida ya kuchezea mipira na kucheza soka la mvuto kutokana na uwanja huo kuteleza.

Aina ya mpira unachezwa inapigwa mipira mirefu, ingawa wakati mwingine mastaa wa Simba wanapojaribu kupiga pasi zao zinawahiwa na wachezaji wa Kagera Sugar.

Wachezaji wanaangukaanguka uwanjani, baadhi jezi zao zikiwa zimechafuka kutokana na matope.

Kwa namna ambavyo hali ya uwanja ilivyo timu itakayotangulia kufunga inaweza kuipa nyingine kurudisha matokeo kirahisi.

Advertisement

Simba safu yake ya mbele, licha ya kufika langoni mwao Kagera lakini inakabwa kutokana kushindwa kujinafasi na pasi walizozoea kucheza.

Paka azunguka uwanja

Wakati wachezaji wakiendelea kupambana dakika ya 27 paka alikuwa anakimbia pembeni ya uwanja na mashabiki walikuwa wanashangilia.

Advertisement