Kwa Kagere mtapata tabu sana

Muktasari:

LIGI Kuu Bara imesimama kwa wiki kama mbili, huku Prince Dube wa Azam akiwa kinara wa mabao na akipewa nafasi kubwa kubebea kiatu cha dhahabu msimu huu, lakini Mzimbabwe huyo kazi anayo kwani inaelezwa straika wa Simba, Meddie Kagere amemzidi ujanja kwa rekodi aliyonayo.

LIGI Kuu Bara imesimama kwa wiki kama mbili, huku Prince Dube wa Azam akiwa kinara wa mabao na akipewa nafasi kubwa kubebea kiatu cha dhahabu msimu huu, lakini Mzimbabwe huyo kazi anayo kwani inaelezwa straika wa Simba, Meddie Kagere amemzidi ujanja kwa rekodi aliyonayo.

Mastaa wa zamani wa kimataifa nchini wameangalia mechi zilizosalia kwa sasa katika ligi hiyo na idadi ya mabao yaliyofungwa hadi sasa na kubaini ni kazi kubwa kwa Dube kuifikia au kuivunja rekodi iliyowekwa na Kagere katika misimu miwili mfululizo iliyopita ya ufungaji mabao.

Kagere aliyesajiliwa Simba kutoka Gor Mahia, aliandika rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kufunga mabao 23 katika Ligi Kuu Bara na kutwaa tuzo ya ufungaji na kuitetea sema msimu uliopita kwa mabao yake 22.

Dude kwa sasa ana mabao 14 akiwa kinara wa ufungaji msimu huu, akimzidi Kagere mabao matatu, huku timu yake ikisaliwa na mechi nne tu, kitu kilichomfanya Ally Mayay na Zamoyoni Mogella kuona ugumu kwa straika huyo Mzimbabwe kuifikia rekodi iliyowekwa na Kagere.

Mayay, aliyewahi kukipiga Yanga na Taifa Stars, alisema ni ngumu rekodi ya Kagere kufikiwa kwa idadi ya mechi zilizopo kabla ya msimu haujaisha, licha ya kukiri kama sio kupata majeraha mara kadhaa Mzimbabwe huyo alikuwa na nafasi ya kushangaza mashabiki wa soka nchini.

“Kwa timu kama Azam, Dube angefikisha kwa sababu, kwani uwanjani wanashambulia sana na huwa hawazuii, ila majeruhi yalimtibulia,” alisema Mayay na kusisita hata Kagere mwenyewe hawezi kuvunja rekodi yake kutokana na nafasi anazopata na jinsi Simba ilivyo. Kwa upande wa Mogella alisema rekodi ya Kagere kufikiwa ni ngumu kwa vile wachezaji kutarudi wakiwa chini kutokana na ligi kusimama ovyo. na labda Kagere mwenyewe angeweza kufika kama angekuwa akipata nafasi ya kucheza.