Kumbe Fei alimpeleka Mudathir Yanga

Pamoja na kutokuwa vizuri kati yake na uongozi wa Yanga, kiungo Feisal Salum Fei Toto alishiriki kumpeleka Mudathir Yahaya kwenye timu hiyo ya Jangwani.

Chanzo cha ndani cha karibu na mchezaji huyo kimesema kuwa, wakati Yanga wanapambana kuhakikisha wanampata kiungo Mudathir baada ya kuwasiliana na uongozi wa timu hiyo, mtu wa kwanza kuwasiliana naye alikuwa Fei ambaye alimueleza kuwa Jangwani ni sehemu bora kwake kwenda.

“Unajua labda Fei anaweza kuwa na matatizo yake mengine lakini kwenye suala la ukweli amekuwa mkweli sana, mfano ukitazama wakati timu ya Yanga ilipokuwa inamtaka Mudathir aliwasiliana na Fei ambaye alimueleza kuwa aende kwenye timu hiyo kwani ni sehemu ambayo anaweza kupata nafasi nzuri ya kucheza,” alisema kiongozi huyo mwenye ushawishi ndani ya Yanga.