Kuiona Azam FC ni sawa na bure

Kuiona Azam FC ni sawa na bure

Unguja. Azam FC leo jioni kuanzia saa 10:00 watacheza mechi yao ya mwisho hatua ya makundi dhidi ya Yosso Boys ambapo viingilio vimeshushwa zaidi.

Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Amaan kisiwani hapa huku kiingilio kikishushwa hadi Sh 1000 kwa mzunguko na Sh 3000 jukwaa kuu.

Awali viingilio vya mechi hizo vilikuwa ni Sh 3000 mzunguko, Sh 5000 na Sh 10000 kwenye majukwaa mengine.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi, Imane Osmond Duwe amesema kuwa mabadiliko ya viingilio hivyo ni kutaka mashabiki wengi waingie kushuhudia mechi hiyi.

Amesema hata hatua ya nusu fainali napo kutakuwa na mabadiliko ya viingilio kulingana na ukubwa wa mechi hasa Simba na Yanga na huenda ikawa Sh 5000, 10000 na 15000.

"Mechi ya leo ni ya mwisho kwenye makundi hivyo tunataka wengi waingie na si kwamba tumezishusha hadhi hizi timu. Nusu fainali na fainali pia kutakuwa na mabadiliko hayo," amesema

Tayari Azam waneingia nusu fainali pamoja na kuwa na mchezo mmoja mkononi, nyingine ni Simba, Yanga na Namungo Fc