KMC yatakata, Mbeya Kwanza hoi

Wednesday June 22 2022
KMC PIC
By Clezencia Tryphone

MABAO manne ya KMC ndani ya dakika 90 yamezidi kulizamisha jahazi la Mbeya Kwanza iliyopanda Ligi Kuu msimu huu.
Beki wa Mbeya Kwanza Geofrey Muha alifungua akaunti hiyo baada ya kujifunga dakika ya 23 na  dakika 57 huku dakika 44 akisababisha penalti iliyopigwa na Matheo Antony baada ya Charles Ilanfya kuchezewa madhambi ndani ya 18.
Dakika ya 53 Habib Kyombo alifunga bao la kufutia machozi ambalo ni bao lake la sita katika msimu huu.
Dakika ya 72 Rolland Msonjo alijifunga akiwa katika harakati za kuokoa na kuzidi kulizamisha jahazi la timu hiyo.
Ilimchukia dakika 64 kocha wa Mbeya Kwanza  Habib Kondo kumuondolea presha ya mchezo Muha na kumtoa na nafasi yake kutwaliwa na Joseph Majagi.

Advertisement