Kibu Denis akingiwa kifua

Kibu kuwamaliza mabosi wake

Muktasari:

  • Kufungwa kwa Simba, hakuondoi ubora wa wachezaji wao ukitaka kuamini hilo hiki ndicho alichokisema nyota wa Mbeya City, kuhusu Kibu Denis

JAPOKUWA Simba imeruhusu kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mbeya City, Kibu Denisi ametajwa miongoni mwa wachezaji walioupiga mwingi lakini haikuwa bahati yao kupata matokeo.

Straika wa Mbeya City, Juma Liuzio amesema Kibu ni mchezaji mpambanaji, kitendo cha timu yake kupoteza mchezo ni kati ya matokeo na hakiwezi kuondoa ubora wake.

"Kufungwa hakumanishi ni timu mbaya, huo ni mpira na una matokeo ya aina tatu, ndio maana nasema Denis ni straika mpambanaji na ataendelea kuisaidia timu yake," amesema na ameongeza kuwa;

"Kama hajafunga dhidi yetu atakwenda kufunga mechi nyingine ndio maana ya ushindani," amesema.

Mbali na hilo, ameuzungumzia mchezo mzima kwamba ulikuwa wa ushindani na malaika wa furaha alikuwa upande wao.

"Ilikuwa mechi ngumu ila jambo la kushukuru ni malaika wa furaha, alikuwa upande wa Mbeya City, sasa tunaangalia majukumu mengine yaliopo mbele yetu,"amesema.