KIBANDA UMIZA: Morrison azua jambo

KITENDO cha nyota wa Simba, Bernard Morrison kuvua bukta uwanjani na kubaki na nguo ya ndani kimchefua mdau wa kibanda umiza na kusema akapimwe akili.

Kile sio kitendo cha kufumbiwa macho, alisema mdau huyo ambaye anafahamika kwa jina la Uswege, “Mimi mwenyewe Simba ila nimechukizwa na kile alichofanya hata kama furaha ilivuka mipaka sio hadi kufikia kiwango cha kuvua nguo, ni ujinga ule.”

Uswege ambaye aliutazama mchezo huo wa fainali akiwa Mwanza aliongeza kwa kusema: “Inawezekana kuna ‘nati’ kichwani zimelegea hivyo wampime wajue namna ya kumsaidia.”