Kassim Dewji amrithi Hans Poppe Simba

Sunday November 21 2021
Kassim PIC

Picha ikiwaonyesha Kassim Dewji akizungumza jambo la Zacharia Hans Poppe enzi za uhai wake.

By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again amemtangaza Kassim Dewji kuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo.

Dewji anachukua nafasi ya Zacharia Hans Poppe aliyefariki miezi kadhaa iliyopita na kuzikwa mkoani Iringa.

Katika mkutano mkuu wa klabu hiyo leo Jumapili, Try Again amesema bodi imempendekeza Dewji kuchukua nafasi ya Poppe.

"Tunafahamu uwezo Dewji, hivyo bodi imemkabidhi jukumu la kuongoza kamati ya usajili ambayo ilikuwa ikiongozwa na Poppe enzi za uhai wake," amesema Try Again.

Advertisement