Karia: Ligi yetu ni namba 8 Afrika kwa ubora

Muktasari:

  • TFF imeingia mkataba wa Sh 3.54 Bilioni wa miaka 10 wa haki ya matangazo ya radio ya  Ligi Kuu na TBC leo Jumanne ambapo kila mwaka utakuwa na thamani ya Sh 300 Milioni.

Ligi ya Tanzania bara imeingia kwenye orodha ya Ligi nane bora barani Afrika.

Mbali na rekodi hiyo, pia Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi 12 zenye matokeo bora.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amebainisha hayo leo wakati akisaini mkataba wa haki ya matangazo ya radio ya Ligi Kuu na Shirika la utangazaji Tanzania.

Amesema Ligi bora haiwezi kuwa na timu moja bora sababu inacheza na timu zingine.

"Ubora wa Ligi yetu ndio umetuweka kwenye orodha ya nchi nane bora, lakini pia kuwa ya 12 kwenye nchi zenye matokeo mazuri.

"Tutaendelea kuhakikisha tunapiga hatua zaidi ya hapa," amesema.