Kagere, Lwanga watinga Simba Day

MSHAMBULIAJI wa Singida Big Stars, Meddie Kagere na kiungo Thadeo Lwanga wametua kwa Mkapa kushuhudia tamasha Simba Day.

Mastaa hao wawili wametua kwa pamoja chanzo cha kuaminika kimeliambia Mwanaspoti kuwa wachezaji hao wamealikwa maalum kwa ajili ya kuwaaga.

Lwanga na Kagere wametemwa na Simba kwenye dirisha hili la usajili kutokana na kushindwa kumshawishi kocha mkuu wa timu hiyo.

Kagere tayari ametambulishwa Singida Big Stars huku Lwanga hadi sasa haijajulikana atacheza timu gani baada ya kumalizana na Simba.