Kagere, Lwanga waagwa kwa heshima Simba

ASANTEE Meddie Kagere na Thadeo Lwanga. Hayo ni maneno ya msemaji wa Simba, Ahmed Ally alipokuwa anawaaga mastaa hao na kuwakabidhi jezi mpya za Simba.

Ahmed ameanza kutaja jina la Kagere ambalo liliibua shangwe kwa mashabiki waliojitokeza kwa Mkapa huku staa huyo akizunguka uwanja mzima kuwaaga mashabiki.

Wakati Lwanga akitajwa jina lake pia liliibuka shangwe ambalo halikukata hadi mastaa hao walipomaliza kuzunguka uwanja kuwapungia mikono mashaniko.
“Wakati waliokuwa wachezaji wetu wakiwaaga mashabiki zao tumeandaa na zawadi zao kwaajili ya kuheshimu mchango wao ndani ya Simba,” anasema

“Asante Kagere asante Lwanga heshima yenu ndani ya Simba itasalia kwenye mioyo ya wanasimba kutokana na mchango wenu,” amesema Ahmed.

Wakati huo huo Lwanga aliwashukuru viongozi kwa nafasi waliyompa ndani ya Simba na kuwatakia kila lakhel kwenye mashindano yaliyo mbele yao.

Kagere aliwashukuru mashabiki na viongozi kwa kufanya kazi nao pamoja kwa muda mrefu na wamefanya mambo mazuri zaidi.