Jezi za Simba msimu uliopita dili kwa Mkapa

PICHA: LOVENESS BERNARD

PAMOJA na Simba kutangaza jezi zao mpya wafanyabiashara wa jezi ambo wamekuwa maarufu kuuza jezi nje ya uwanja wamekiri kukosa mzigo mpya jezi na kuamua kuuza za msimu uliopita.

Wakizungumza kwa nyakati tofuti walisema msimu huu wamekutana na ugumu kutokana na mzigo ulioingia kuwa mchache

Jumanne Elifadhil anasema alipata jezi nane ambazo alizimaliza muda huohuo aliozipata hivyo leo ameamua kuuza za msimu uliopita ambozo pia zinauzika.
"Kupata mzigo mpya kwa wingi wa mashabiki waliojitokeza dukani jana na duka lilikuwa moja tu wametunyima pesa,"
Eliamin Brown alisema kukoseka kwa jezi mpya kumewafanya wamalizie mabaki ya jezi ya msimu uliopita huku changamoto ikiwa ni mdhamini aliyemaliza mkataba na timu hiyo.

"Jezi zinauzika hii ni kutokana na kukoseka kwa jezi za msimu mpya shida iliyopo ni kubandua nembo ya mzamini wa zamni," anasema.