Jeremiah Juma afunga ‘hat-trick’ ya kwanza Ligi kuu NBC

Saturday November 27 2021
Jeremiah PIC
By Saddam Sadick

Mbeya. Mshambuliaji wa Tanzania Prison, Jeremiah Juma amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu 'hat-trick' kwenye Ligi Kuu ya NBC 2021/22.

Jeremiah amefunga mabao hayo wakati timu yake ikichuana na Namungo katika uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa, hadi mapumziko timu hizo zinaenda mapumziko Prison wakiongoza 3-0.

Tanzania Prisons ilipata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Mbeya Kwanza waliposhinda mabao 2-1 na kabla ya hapo ilikuwa imecheza mechi tano bila kuonja ladha ya ushindi.

Mshambuliaji Juma ndiye amekuwa shujaa wa mechi hiyo hadi mapumziko baada ya kutupia mabao yote na kuiweka pazuri timu hiyo.

Nyota huyo alianza kufunga bao mapema dakika ya nne, kisha dakika ya saba na dakika ya 14 na kufikisha mabao manne hadi sasa.

Namungo iliingia uwanjani ikikumbuka sare waliyopata dhidi ya Yanga, hivyo kuhitaji ushindi leo ili kutuliza presha.

Advertisement
Advertisement