Jeremiah: hii Simba mbona inafungika

STRAIKA wa Tanzania Prisons, Jeremiah Juma amesema sehemu pekee ya kujinusuru wasishuke Ligi Kuu Bara ni kwenye mechi ya leo dhidi ya Simba na wala sio ile ya mwisho na Ruvu Shooting itakayopigwa Jumatano ijayo.

Jeremiah mchezaji pekee mwenye hat trick katika ligi hiyo alisema kuna unafuu wa kupata matokeo kama wataikazia Simba, kuliko Ruvu inayopambana nao kuepuka kushuka daraja.

“Sina maana Simba ni timu mbaya, ninachoangalia angalau haitakuwa mechi ya kukamiana kama tutakavyokutana na Ruvu inayopigania kusalia Ligi Kuu.

“Tukipoteza mambo yatakuwa ni magumu zaidi maana tuko nyumbani na tunaenda kumaliza ugenini dhidi ya Ruvu Shooting, kifupi tutapambana kwa jasho hadi tone la mwisho,” alisema Jeremiah.