Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu za Mwamnyeto zafichuka

KUMBE nidhamu anayoionyesha beki wa Yanga, Bakari Mwamnyeto ambaye ni nahodha msaidizi wa Lamine Moro, inatokana na baba yake mzazi aliyefichua siri uwa imeanzia kwenye misingi aliyoijenga ndani ya familia yake.

Baba mzazi wa beki huyo, Mwamnyeto Nondo alisema kuna misingi ambayo aliijenga katika familia yake ambayo kijana wake hatakiwi kuivunja hata kama yupo nje ya familia hiyo.

Alisema aliwafundisha namna nidhamu unavyoweza kumpa hatua ya maendeleo na akaonekana bora katikati ya wengine, jambo alilosema linaenda sawa mpaka sasa kwani, anafuatilia kila anachokifanya uwanjani.

“Nilianza kuwafundisha nidhamu tangu wakiwa wadogo kwa kila kitu walichokuwa wanakifanya hapa nyumbani kabla ya kuvuka mipaka ya familia nyingine, naamini Yanga wasingekurupuka kumpa beji hiyo angekuwa hajielewi,” alisema na aliongeza kuwa,

“Niliposikia kapewa unahodha nilifarijika sana, nikampigia simu kumwambia uongozi unahitaji busara ili kutatua mambo na kuwafanya wenzake wakiwa wamoja na sio kujiona yeye ndiye yeye,” alisema.

WANAFURAHIA MAISHA

Alisema mbali na nasaha anazompa beki huyo, kumsisitiza aelekeze nguvu kwenye kazi yake ambayo ndio fungu lake, pia amekuwa kijana bora kwao kwa kuwasaidia kimaisha.

“Kawa kijana mzuri, anapopata chochote huwa anatutumia mimi na mama yake, tunajivunia yeye na tunamuomba Mungu asiache mafunzo tuliompa tangu akiwa mtoto, aendelee hivyo ili aweze kufika mbali zaidi,” alisema.

Mbali na hilo, aligusua mchezo wa watani wa jadi kwamba, kama kijana wake atapata nafasi ya kupangwa na kocha kuanza kikosi cha kwanza, atatakiwa kutumia muda mwingi kufanya kazi kuliko kucheza na jukwaa.

“Ni mchezo ambao una mambo mengi sana kama tunavyofahamu, lakini ataandika heshima kama atatumia muda wake mwingi kuibeba timu na kuwaachia mashabiki kufanya kazi yao na sio yeye aanze kutaka sifa za kushangiliwa. Anapaswa kufanya kazi yake vizuri kwa kuwa ndio itakayompa heshima. Mwisho wa siku mashabiki wake wanataka kuondoka uwanjani wakiwa na furaha ya ushindi hivyo, lazima apambane sana na kwa umakini,” alisema.