Infantino kuongeza nguvu AFCON

Infantino kuongeza nguvu AFCON

ARUSHA. Rais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA), Gianni Infantino amesema chini ya uongozi wake atahakikisha anaipa nguvu mashindano ya AFCON ili yawe makubwa zaidi.

Akiongea katika mkutano mkuu wa CAF ambao unaendelea kwa sasa katika ukumbi wa mikutano ya Kimataifa ya Arusha AICC, amesema anaamini kupitia uongozi wake Afrika utandaa mashindano makubwa ya ambayo yanasimamiwa na FIFA.

Ameongeza kuwa amepanga kuipa nguvu mashindano ya AFCON ambayo yanasimamiwa na CAF hili kuwa na nguvu pamoja na ubora mkubwa tofauti na ilivyo kwa sasa.

"Afrika ina vipaji vingi sana wana wachezaji wanacheza mashindano makubwa kama kwenye vilabu vikubwa duniani kama UEFA na mengine mengi hivyo ni muda wa kuendelea kuipa nguvu soka la Afrika". amesema Infantino.

Infantino pia ameisifia jiji la Arusha ambayo imeandaa mkutano wa CAF kutokana na mazingira na hali ya hewa yake nzuri na kuweka wazi kuwa hii ni mara yake ya pili anakuja Tanzania.