Hitimana kuchukua mikoba ya Gomes

Saturday September 11 2021
HITIMANA PIC
By Saddam Sadick

Kocha Hitimana Thiery raia wa Burundi amethibitisha kujiunga na Simba na muda mchache ujao atatangazwa rasmi na bingwa huyo mtetezi wa Ligi Kuu Bara.

Thiery alitua siku mbili nchini akitokea kwao Rwanda, ambapo safari yake ilikuwa ni kurudi Mtibwa Sugar aliyokuwa amewahi kuitumikia katikati ya msimu kisha kung'atuka kwa madai ya kutoelewana na wasaidizi wake kwenye benchi la ufundi.

Thiery ameithibitishia Mwanaspoti kuwa tayari ameshamalizana na Wekundu hao na kwamba muda wowote watamtangaza.

Hitimana anachukua nafasi ya Didier Gomes ambaye ametangazwa kutokuwa na sifa za leseni itakayomfanya kuinoa timu hiyo kimataifa.

Advertisement