Hersi avunja ukimya utata wa urais Yanga, GSM

Hersi avunja ukimya utata wa urais Yanga, GSM

Muktasari:

  • Mgombea urais wa klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said amevunja ukimya kuhusu wasiwasi wa baadhi ya wadau wa soka endapo atakuwa rais wa klabu hiyo na wakati huo huo mtumishi wa GSM kutasababisha  mgongano wa kimaslahi.

Mgombea urais wa klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said amevunja ukimya kuhusu wasiwasi wa baadhi ya wadau wa soka endapo atakuwa rais wa klabu hiyo na wakati huo huo mtumishi wa GSM kutasababisha  mgongano wa kimaslahi.

Hersi ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM na mgombea pekee wa urais kwenye uchaguzi mkuu wa klabu ya Yanga wa Julai 9.

Hivi karibuni kumekuwa na maswali kwa baadhi ya wadau wa Soka kuhusu nafasi ya Hersi kama atapewa ridhaa ya kuwa rais wa klabu hiyo na wakati huo huo ni mtumishi wa GSM ambao ni wafadhili wa klabu hiyo.

"Imekuwa ni mjadala huko mtaani, lakini kuwepo kwangu GSM hakutakuwa na mgongano wa maslahi kama nitapewa ridhaa ya wanachama ya kuwa rais kwenye uchaguzi mkuu". amesema Hersi na kuongeza.

Amesema kuwepo kwake GSM hakuitaipa upendeleo kampuni hiyo kwa chochote Yanga.

"Kwenye mchakato wa mabadiliko, katiba yetu imetoa asilimia 49 kwa wawekezaji wanne, zitafanyiwa utaratibu kabla ya wawekezaji kupewa". amesema Hersi na kuongeza,

"Mchakato utaanza kwa kutangaza tenda kutafuta kampuni itakayoithaminisha klabu, hatakuja mtu kununua hisa sababu ya upendeleo wangu, bali kwa kufuata taratibu zote, hivyo kwenye hili hakutakuwa na conflict of interest 'mgongano wa kimaslahi".

Akitolea mfano faida na hasara za klabu kumilikiwa na wanachama na watu binafsi, amesema katika mfumo wa mabadiliko walijifunza yote hayo.

Faida klabu kuwa ya wanachama, inakuwa na uhusiano na mapenzi na wanachama wake.

"Hasara yake, klabu inakosa dirisha la uwekezaji, ile inayomilikiwa na watu binafsi hazina mapenzi na wanachana lakini faida yao inakuwa na uwekezaji mkubwa.