GSM yataja sababu kudhamini Ligi Kuu

Tuesday November 23 2021
gsm pic
By Waandishi Wetu

Kampuni wa GSM, imeingia mkataba wa miaka miwili na Ligi Kuu Bara wenye thamani ya Sh2.1 Bilioni kama mdhamini mwenza.

Mkataba huu umesainiwa na Makamu wa kwanza wa Shirikisho la soka la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Athumani Nyamlani pamoja na Mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM, Hersi  Saidi.

Akizungumza katika mkutano huu Mkurugenzi wa uwezeshaji wa kampuni ya GSM, Hersi amesema mkataba huu utakwenda kuzinufaisha moja kwa moja timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara.

“Kampuni ya GSM imeona inayosababu ya kuendelea kuisapoti tasnia ya mpira wa miguu Tanzania kwa kuongeza nguvu ya udhamini katika Ligi jambo ambalo litachochea ukubwa ligi yetu,” amesema na kuongeza;

“Pia tunapongeza juhudi zinazofanywa na Bodi ya ligi kuhakikisha ligi inapata hatua hivyo kama wadau wa soka nchini lazima tuwaunge mikono,”

“Mkataba  huu naimani utakwenda vizuri kama vile ambavyo matumaini yetu yalivyo kwani tunaamini katika uongozi wa sasa wa TFF ndio maana tumefanya uwekezaji huu.”

Advertisement

Aidha pia mkurugenzi huyu amedaini Kua mkataba huo hauna mahusiano yoyote na timu zinazothaminiwa na kampuni hiyo.

“Ukutakua na upangaji wowote wa matokeo kupitia mkataba huu bali lengo ni kuona kila timu kuishiriki vyema Ligi bila changamoto za kiuchuni,” amesema  Hersi.

Kwa upande wa Nyamlani amesema anaishukuru kampuni ya GMS kua mdhamini mwenza ambao wameufanya.

“Mkataba huu utakua na manufaa makubwa kwa timu zetu kwani utaweza kwenda kutatua changamoto mbalimbali hata hivyo uongozi wa TFF, umejipanga kutumia  vyema fedha zinazowekwa na wadhamini wetu”

“Hivyo tuwaunge mkono GSM kwa ajili ya kuendelea kuisapoti ligi yetu na pia wadau wengine wa wajitokeze kuidhamini na kufanya uwekezaji kama hivi au zaidi,” amesema Nyamlani.

Advertisement