Gomes ahusika na usajili wa nyota hawa

Simba tayari imesajili wachezaji wanne ambao ni kipa Jeremiah Kisubi, beki Israel Mwenda, winga Jimson Mwinuke na straika Denis Kibu.

Lakini pia leo inatarajia kumpokea Mmalawi, Peter Banda ambaye jina lake limepitishwa na Kocha wa timu hiyo Didier Gomes.

Gomes akiwa Ufaransa kwa mapumziko, aliliambia Mwanaspoti kuwa, jina la Banda lilitua mezani mwake na kuanza kumfuatilia.