Gomes afanya mabadiliko manne dhidi ya Kagera

KOCHA wa Simba, Mfaransa Didier Gomes amefanya mabadiliko katika kikosi cha kwanza kwa kuwaanzisha wachezaji watatu ambao hawakupata nafasi katika mchezo uliopita.

Mchezo uliopita dhidi ya Simba walicheza dhidi ya Mwadui katika Uwanja wa Kambarage Shinyanga na kushinda bao 1-0, ambalo lilifungwa na nahodha, John Bocco ambaye ameanzia benchi leo.

Wachezaji hao wanne ambao wameanza katika kikosi cha kwanza cha Simba, ambacho jioni ya leo kitacheza dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba, Hassan Dilunga, Mzamiru Yassin, Chriss Mugalu na Luis Miquissone.

Katika mechi hiyo ya Mwadui Dilunga, Mugalu na Miquissone hawakucheza kabisa wakati Mzamiru aliingia kipindi cha pili akitokea benchi.

Kikosi cha Simba kimeanza na kipa, Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein 'Tshabalala' Joash Onyango, Pascal Wawa, Taddeo Lwanga na Dilunga.

Wengine Mzamiru, Mugalu, Clatous Chama na Miquissone.

Katika benchi la wachezaji wa akiba wapo, Erasto Nyoni, Rally Bwalya na Meddie Kagere ambao hawa wote walianza katika mechi iliyopita.

Wengine Benno Kakolanya, Ibrahim Ame, Ibrahim Ajibu na nahodha, Bocco aliyeingia kipindi cha pili na kufunga bao pekee ambao lilikuwa la ushindi.

Wakati kikosi cha Simba, kikianza hivyo wenyeji wao Kagera Sugar, walianza na Ramadhani Chalamanda, Mwaita Gereza, David Luhende, Abdallah Mfuko, Ally Mtoni 'Sonso',

Wengine Nassoro Kapama, Yusuph Mhilu, Ally Nassoro, Peter Mwalyanzi, Abdul Kassim na Erick Mwijage.

Katika benchi la wachezaji wa akiba wapo, Mlekwa, Yusuph Mlipili, Dickson Mhilu, Hassan Mwaterema, Kibilige na Abbdal Seseme.